Wachezaji wanaotakiwa kuhamia timu kubwa Ligi Kuu

Wachezaji wanaotakiwa kuhamia timu kubwa Ligi Kuu


Kuna kundi kubwa la wachezaji wapo klabu ndogo Ligi Kuu Tanzania ila wana uwezo wa kucheza timu kubwa za Simba, Azam na Yanga, kuna baadhi ya nyota wapo kwenye hizi  klabu ndogo il wana uwezo mkubwa kuliko wachezaji wanao kipiga hizi katika timu kubwa

Miaka yote klabu za Simba na Yanga zimekuwa zikitegemea timu hizi ndogo kusajili wachezaji wao ambao baadae wanakuja kuibuka nyota hapa nchini, watu kama Ngassa, Kichuya, Msuva, Mohamed Hussein, Juma Abdul na wengine wote walitokea timu ndogo na kuibukia Simba na Yanga ambapo ndipo walipo enda kutengeneza majina

Katika michezo 16 ya Ligi Kuu tayari kuna baadhi ya wachezaji wameonesha dalili kubwa ya kuja kuhamia klabu kubwa kwa misimu ya hivi karibuni kama kasi yao ikiendelea hivyo hivyo
chapu news inakuletea orodha ya wachezaji wa kitanzania wanaotakiwa hamia klabu kubwa kutokana na kiwango vyao bora kwa msimu huu

Rashid Mandawa-Mtibwa Sugar

Mshambuliaji huyu kutoka klabu ya Wakata miwa wa Morogoro, Mandawa ameanza msimu kwa kasi hadi sasa amepachika magoli 7 magoli 2 nyuma ya kinara wa ufungaji, uwezo wa kufunga kwa  straika huyu ni mkubwa kuliko hata baadhi ya washambuliaji waliopo katika klabu za Simba, Azam na Yanga.

Omar Mponda-Ndanda

Kwa kipindi fulani wana Msimbazi walishawahi kuulizia huduma ya mshambuliaji huyu, Mponda ana nguvu ya kupambana na walinzi hata wawili na zaidi pia ni mzuri kwenye kufunga magoli ya kichwa, nafasi yake ni finyu kubaki kwenye klabu yake ya sasa hapo mwakani kama akiendelea na kasi yake

Riffat Khamis-Ndanda

Amefanikiwa kutengeneza kombinesheni bora na mwenzake Mponda katika klabu yao, kwa pamoja wamefunga magoli zaidi ya 10, Khamis kiumri bado ni mdogo na nafasi yake ni kubwa kupiga hatua kisoka

Said Kipao- JKT Ruvu

Mlinda mlango wa JKT Ruvu amekuwa na mwanzo mzuri tangu mwanzo mwa msimu, uimara wake mkubwa wa kuzuia makombora langoni mwake kumempa umaharufu hapa nchini, Kipao tayari ameteuliwa kwenye timu ya Taifa chini ya Mkwasa baada ya kiwango bora kwenye mechi za Mzunguko wa kwanza

Raphel Daudi- Mbeya City

Ukitaja wachezaji watatu bora kwenye timu ya Mbeya City msimu huu jina la Raphael Daud litakuwa mbele, kiungo huyo mshambuliaji ametikisa nyavu mara 3 na kusaidia magoli zaidi ya 5 kwa wenzake ni dhahiri itakuwa ngumu kwa miamba hao wa dimba la Sokoine kumbakiza kuendelea kuitumikia klabu yao kwa msimu ujao.

Abdulahman Mussa- Ruvu Shooting

Ndiye mfungaji wa goli la kwanza kwenye uwanja wa uhuru baada ya kufungwa muda mrefu kupisha matengenezo, Mussa mfungaji bora kwenye kikosi cha Ruvu Shooting akiwa na magoli matatu msimu