Samatta Aambiwa na Baba yake

Chagua Klabu inayolipa vizuri, Samatta Aambiwa na Baba yake

 Habari ya Mbwana Samatta kwenda Ubelgiji bado ina utata na haijakaa vizuri, Baba yake, Mzee Ally Samatta amemshauri mwanaye kuchagua klabu itakayomlipa vizuri
Mbwana Samatta, mchezaji wa Tanzania 
Goal imegundua kuwa kauli hiyo ya Mzee Samatta imeibuka baada klabu mbili za Ubelgiji kuonyesha nia ya kutaka kumsajili kijana wake.

Klabu ya kwanza ni KRC Genk, ambayo kwa heshima mkataba wa awali umesainiwa ili kumruhusu mchezaji huyo kujiunga nayo baada ya mkataba wake na TP Mazembe kukoma ifikapo Aprili mwaka huu.

Hata hivyo mchakato huo umeonekana kukumbwa na vizuizi baada ya TP Mazembe kuripoti kuwa imepokea ofa nzuri zaidi iliyochangamka kutoka kwa Standard Liege ambayo imemaliza nafasi ya nne katika Ligi ya Ubelgiji. KRC Genk ilimaliza nafasi ya saba.

Mzee Samatta akaririwa na The Citizen:

 “Mimi kama baba wa mchezaji, naona ugumu katika mambo haya, lakini shauku yangu kuu ni kuona kijana wangu akifanikiwa kama mchezaji anayecheza Ulaya. KRC Genk imeeleza mikakati. Viongozi wake walikuja Tanzania wakaongea na mimi na mchezaji pia. Walimfuata Mbwana hadi Japani na akasaini mkataba wa awali. Lakini inaonekana bosi wa TP Mazembe, Moise Katumbi hakubaliani na biashara hii, anamtaka Mbwana kujiunga na Standard Liege badala yake.”

Aliongeza: “Siwezi kuingilia mambo yao, kwa sababu TP Mazembe ndio waliomwezesha kijana wangu kufikia hadhi aliyo nayo sasa. Namheshimu Katumbi kwa sababu alichangia sana mafanikio ya Mbwana. Ushauri wangu kwake ni kuangalia klabu nzuri kwa sababu soka ni ajira”
Alieleza zaidi kuwa inaonekana kijana wake anazidi kuchanganyikiwa kwa sababu hataki ndoto zake zizimike, ingawa bado hajalipwa kitu na Genk, kinyume na washika dau wengine wa soka wanavyofikiri.

Mzee Samatta aliendelea: “Mwanangu ndiye muhusika mkuu katika swala hili; yeye ndiye mwenye uamuzi wa mwisho ni wapi anataka kwenda, ingawa natambua kwamba kuna faida nyingi za kujiunga na Genk kutokana na historia yake. Waafrika wengi wamefanikiwa kucheza kwenye timu za klabu kubwa Ulaya, hasa Uingereza wakitokea klabu hiyo.

“Ni pamoja na Thibaut Courtois na Kevin De Bruyne waliojiunga na Chelsea na Christian Benteke ambaye alijiunga na Aston Villa na sasa anacheza Liverpool.”

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »