Samatta ametambulishwa Genk

Samatta ametambulishwa Genk na kupewa jezi namba 77

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na mchezaji bora wa ndani wa Afrika Mbwana Samatta ametambulishwa rasmi na ameshakabidhiwa jezi na klabu ya Genk
Samatta Genk
Samatta amepewa jezi nambari 77 alipokuwa akitambulishwa mbele ya waandishi wa habari Ubelgiji ambapo amesaini mkataba wa miaka minne.

Kwa mujibu wa mtandao wa klabu ya Genk, Samatta amesaini mkataba unaomalizika msimu wa mwaka 2019-2020.

Samatta amejiunga na Genk akitokea TP Mazembe ambapo alicheza kwa miaka mitano (5) tangu mwaka 2011 alipojiunga na klabu hiyo akitokea klabu ya Simba SC hadi mwaka 2015.

Mkataba wa Samatta na Mazembe ulikuwa unamalizika mwezi April mwaka huu lakini tayari amesaini mkaba mpya na klabu hiyo ya barani Ulaya.

Aidha Samatta ameishukuru klabu ya TP Mazembe pamoja na mmiliki wa klabu hiyo Moise Katumbi kwa kukuza kipaji chake.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »