Je! Manchester United itaweza kupindua historia leo Darajani?
Eden Hazard anatarajiwa kuwemo kwenye kikosi cha Chelsea kitakachoivaa Manchester United katika uwanja wa Stamford BridgeMabingwa watetezi watakuwa wakitafuta uamsho chini ya kocha wa muda Guus Hiddink, ambaye ameiongoza klabu kucheza mechi nane bila kufungwa tangu alipochukua mikoba ya Jose Mourinho katika dimba la Stamford Bridge.
United kwa upande mwingine wamefurahia mwamko wao, na ari mpya baada ya kuitungua Stoke City katikati ya juma na kupunguza presha mabegani mwa Louis van Gaal.
Louis van Gaal bado hana kikosi cha uhakika cha kwanza anapokwenda kutafuta ushindi wa kwanza dhidi ya Chelsea tangu akalie kiti cha moto Old Trafford.
Beki Phil Jones (mwenye jeraha la kifundo cha mguu) yu karibu kurejea mzigoni, lakini mchezo huo wa Stamford Bridge umemjia mapema sana.
Takwimu Opta
Chelsea hawajafungwa katika mechi zao sita za mwisho walizowahi kucheza Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Manchester United (W3 D3).
Manchester United wamefungwa mara nyingi na Chelsea kuliko mpinzani mwingine yeyote katika zama za Ligi Kuu ya Uingereza (mara 16).
Manchester United wameshinda moja tu kati ya mechi 13 walizocheza katika uwanja wa Stamford Bridge Ligi ya Uingereza (W1 D4 L8).
Chelsea wamesare katika mechi zao tatu za mwisho katika uwanja wa Stamford Bridge - hawajawahi kutoa sare mara nne mfululizo katika ardhi ya nyumbani katika historia ya michuano.
Utabiri wa Mwandishi
Mechi kubwana kwa namna hii tunakwenda kuhitimisha wikiendi - Mechi kali ya Jumapili Kuu! Chelsea hawajawa na mechi kubwa na muhimu kama hii - wana shauku ya kurejea nne bora - Nashangaa kwanini walishindwa kuiteketeza Watford kurahisisha safari yao ya matumaini. Mashabiki wengi walivunjika moyo.
Kwa mechi hii ya leo natabiri Chelsea 3-2 Manchester United
EmoticonEmoticon