Jose Mourinho atamtema Juan Mata atakapotua Manchester United
Jose Mourinho anajiandaa kumtema Juan Mata tena
atakapokuwa kocha wa
Manchester United wakati tetesi za
kutua Old Trafford zinapozidi kupamba
moto
Kocha huyo wa zamani wa Chelsea yupo katika mazungumzo yaliyochangamka sasa kuchukua kibarua cha Manchester United na ameshamtaarifu Mkurugenzi mtendaji Ed Woodward kuwauza viungo hao wawili.
Mata aliuzwa Januari 2014 kutoka Chelsea, Fellaini ameshindwa kufanya kazi nzuri aliyotarajiwa kuifanya Manchester United tangu atue Old Trafford akitokea Everton.
Mourinho ambaye hajataka kuficha dhamira yake kutaka kuinoa Manchester United, ameainisha kikosi anachokitaka katika mikutano yake na Woodward.
Mreno huyo ndiye aliyechochea Mata auzwe kutoka Chelsea wakati David Moyes alipokuwa mzigoni Old Trafford.
Ingawa Mata alitajwa kwenye timu ya PFA ya mwaka 2013, Mourinho aliidhinisha kuuzwa nyota huyo kutoka Chelsea Januari 2014 na akauzwa Manchester United kwa kitita cha paundi milioni 37.
Mata haendani na mipango ya Mourinho katika Old Trafford na atataka winga huyo wa Kihispania kuonyeshwa mlango wa kutokea mara moja kabla hajachukua majukumu ya kuinoa klabu hiyo.
Fellaini naye atakuwa katika mkumbo huo wa kuondoka endapo makubaliano ya Mourinho kuchukua kiti cha Van Gaal yatafikiwa.
Mourinho atapewa fedha kwa ajili ya kuunda kikosi anachokitaka ili kuweza kushindana vema na
Manchester City, Chelsea na Arsenal msimu ujao kama zali litakuwa upande wake.
EmoticonEmoticon