Azam FC kikaangon tena dhidi ya Mwadui FC Ligi Kuu
Azam FC Jumapili itakuwa nyumbani uwanja wa Azam Complex, kuwakabili Mwadui FC, ukiwa ni mchezo wa mzunguko wa 16 wa Ligi ya Vodacom TanzaniaKatika mchezo wa kwanza ulichezwa Mwadui Complex Azam FC, walishinda bao 1-0 na sasa Mwadui watakuwa na kazi ya kuonyesha ubora wao kwa kulipa kipigo hicho.
Azam itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na ari baada ya kuwa mabingwa wa michuano maalumu waliyokwenda kushiriki huko Zambia niwazi wangependa kuitumia kasi hiyo kushinda mchezo huo na kurudi kileleni mwa msimamo wa ligi kutoka nafasi ya tatu waliyopo hivi sasa.
Kocha Stewart Hall ni wazi amewaambia wachezaji wake ugumu uliopo kwenye mchezo huo hasa ukiangalia uimara wa kikosi cha Mwadui ambacho kinaundwa na wachezaji wengi waliocheza timu kubwa nchini na kushiriki michuano mbalimbali ya kimataifa.
Ingawa Hall atakuwa ana advantegi ya kuwa nyuma kwa michezo miwili lakini hilo halijalishi kutokana na ushindani uliopo kwa sasa kwani aliweza kupoteza nafasi ya uongozi wa ligi kwa kulazimishwa sare ya 1-1 na African Sports inayoshika nafasi ya mwisho akiwa nyumbani.
Kikosi cha Mwadui kimeshawasili Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo huo na kocha wake Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amepania kuhakikisha wanashinda mchezo huo baada ya kupoteza mchezo uliopita kwa kufungwa bao 1-0 na African Sport.
Julio amesema anaijua vizuri Azam ni timu ngumu lakini anajivunia ubora wa kikosi alichokuwa nacho msimu huu kinauwezo mkubwa wa kufanya vizuri na timu yeyote ambayo watakuna nayo hivi sasa.
“Azam ni timu nzuri lakini hilo halitufanye tuwaongope tunawachukulia kama zilivyo timu nyingine siye tumejipanga kucheza na timu yoyote na lengo letu la kwanza ni ushindi kitu ambacho sioni kama kinashindikana kutokana na ubora wa timu yangu,”amasema Julio.
Kipigo cha jana dhidi ya African Sports kimeiweka Mwadui nafasi ya tano ikiwa na pointi zake 28 katika michezo 17 iliyocheza hivyo inalazimika kupambana ili kupata ushindi ili kuendelea kuifukuzia Mtibwa Sugar iliyopo juu yake ingawa siyo kazi rahisi kutokana na ushindani uliopo.
EmoticonEmoticon