Barcelona imeweka rekodi mpya baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Valencia
Goli la kusawazisha la Wilfrid Kaptoum sio tu liliwanyima ushindi
Valencia iliyo chini ya Garry
Neville lakini pia limeiwezesha Barcelona
kuweka rekodi mpya
Baaada ya sare hiyo Barcelona imeweka rekodi ya kucheza mechi 29 bila kufungwa.
Barcelona chini ya kocha ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa timu hiyo Luis Enrique hawajapoteza mchezo katika mashindano yote wanayoshiriki tangu Oktoba 3, na kufanikiwa kuvunja rekodi iliyowekwa na Pep Guardiola msimu wa 2010/11 wakati akiifundisha klabu hiyo.
Mara ya mwisho Barcelona walifungwa na Sevilla, ikiwa imeshapita miezi minne sasa.
Enrique aliifikia rekodi ya Guardiola wakati huohuo akiwa anatimiza michezo 100 katma kocha wa klabu hiyo, huku akisema hicho hakikuwa kipaumbele chake.
“Msimu utakapomalizika, nitawajulisha kama tumefanya kitu chanya”, alisema Enrique pale Barca ilipokuwa imetimiza michezo 28 bila ya kufungwa wakati wallipocheza dhidi ya Levante.
“Ni vizuri zaidi kucheza michezo 100 kuliko 50, lakini mimi siangalii namba. Kikubwa kinachonivutia nini umoja uliopo ndani ya wachezaji ambao unaleta matokeo chanya”.
Barcelona watajaribu kuongeza rekodi yao ya kutofungwa michezo 30 watakapokuwa wakipepetana na Celta Vigo, klabu ya zamani aliyokuwa akiinoa Luis Enrique, ambayo iliwafunga mwanzoni mwa msimu, katika mchezo huo, washambuliaji wao hatari Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar watakuwa wamesharudi.
EmoticonEmoticon